Enock Maregesi Quote #1
A.K.A kirefu chake ni 'Also Known As'. K.K.K kirefu chake ni 'Kadhalika Kikijulikana Kama'. K.N.K kirefu chake ni 'Kadhalika Nikijulikana Kama'. K.A.K kirefu chake ni 'Kadhalika Akijulikana Kama'. Kadhalika, unaweza kusema P.K.K (Pia Kikijulikana Kama), P.N.K (Pia Nikijulikana Kama) au P.A.K (Pia Akijulikana Kama).Tujifunze kuupenda utamaduni wetu, ili vizazi vijavyo visisumbuke.
Enock Maregesi Quote #2
Acha alama katika dunia baada ya kuondoka.
Enock Maregesi Quote #3
Adam Kuambiana umerudi nyumbani ulikotoka, ukiongozwa na imani na mwanga wa wale uliowapenda na kuwapoteza. Hatuwezi kukumbuka kwamba umetutoka bila kukumbuka kwamba uliishi, na kwamba maisha yako yalitupa kumbukumbu nzuri tusizoweza kuzisahau haraka. Jumanne, siku ya kuuaga mwili uliokuwa ukitumiwa na wewe, wengine watasema Kwa heri lakini mimi nitasema Asante! Asante kwa sababu ya kipaji chako. Asante kwa sababu ya kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wako wote, kutoa sauti kwa wale wote waliokuwa hawawezi kusikika. Asante kwa sababu ya kuacha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta wakati ukiingia, na Asante kwa sababu ya maisha yako. Tukiendelea kuomboleza kifo cha Adam Kuambiana hapa duniani, wengine wanasherehekea kukutana naye huko mbinguni. Mchungaji wa uhai wa wote Mungu wa mbinguni ailaze roho yake mahali pema peponi: Yeye ni mwandishi wa hadithi ya maisha yetu na ndiye aliyeandika ukurasa wa mwisho wa hadithi ya Adam.
Enock Maregesi Quote #4
Afrika imekaliwa na mizimu. Wazungu hawataweza kumaliza mali ya Afrika. Mali ya Afrika ni ya Waafrika wenyewe. Itamalizwa na sisi wenyewe.
Enock Maregesi Quote #5
Afrika isomeshe watu wake, na itumie vizuri mapato yanayotokana na mauzo ya rasilimali zake kwa faida ya jumla ya wananchi wa nchi zake, kusudi baadaye wawe wataalamu wa rasilimali za nchi zao wenyewe, kuepukana na utumwa wa rasilimali. Rasilimali za Afrika zina miiko na masharti yake.
Enock Maregesi Quote #6
Akili yako isipokuwa timamu, familia itakushinda. Familia ikikushinda utalaumiwa na Mwenyezi Mungu.
Enock Maregesi Quote #7
Amani ya nafsi ni zaidi ya amani ya kisiasa. Amani ya kisiasa itaweza kupatikana endapo watu watakuwa na amani ndani ya mioyo yao. Watu wakiithamini amani na kuielewa watayafurahia maisha yao, na mataifa yakiithamini amani na kuielewa yatastawi. Vita hutengenezwa ndani ya mioyo ya watu. Ukiitafuta amani ndani ya moyo wako, taifa halitasimama kupigana na taifa, amani itaweza kupatikana.
Enock Maregesi Quote #8
Baada ya Adam na Hawa kutenda dhambi katika bustani ya Edeni, kila mtu anayezaliwa anazaliwa katika dhambi. Kwa hiyo dhambi hutokana na maisha, na maisha hutokana na dhambi.
Enock Maregesi Quote #9
Baada ya kelele zile Murphy alijisemea moyoni kama angebaki pale alipokuwa amebana au angetoka, washenzi wangemvua nguo; alitaka akimbilie nje lakini akasita. Nje wangeweza kumwona na hivyo kumuua wakati sasa alishaanza jitihada za kuokoa maisha yake. Alipofikiri kwa sana aliamua liwalo na liwe. Alikurupuka akajirusha nje, ambako chapuchapu alinyanyuka na kuangaza sehemu zote lakini bila kuona adui hata mmoja. Tumaini la kushinda likamwendea ghafla na kumsukuma mbele. Alikimbia mpaka kona ya kaskazini-mashariki na kubana, baada ya kusikia vishindo vya watu wakikimbia. Kwa jicho la haraka aliangalia magharibi, akaangalia tena saa na kuona kumbe alikuwa bado na muda; dakika sita wakurugenzi wangefika na upande wa magharibi hakukuwa na mtu. Murphy alishtuka baada ya kuhisi mtu karibu yake. Yule mtu alijitokeza kwa kasi, lakini ikawa bahati sana mbaya kwake. Murphy alimvuta kama mtego wa samaki, kwa mkono wake wa kushoto; akamminya kichwa kwa kidole gumba, na kumkabidhi kareti nzito ya shingo. Alipomwachia alijipiga chini kama gunia, akapoteza fahamu.
Enock Maregesi Quote #10
Badilisha tabia. Badilisha mazingira ya maisha yako. Haijalishi una umri kiasi gani au wewe ni mwanamke au mwanamume, bado hujachelewa kubadili maisha yako kutoka duni kuwa bora – kuwa na amani, furaha na kuridhika. Kama desturi yako ni kuamka saa 12:00 asubuhi kila siku ili ufike kazini saa 2:00 asubuhi ambao ni muda wa serikali wa kuanza kazi, amka saa 11:30 asubuhi ili ufike kazini saa 1:30 asubuhi – nusu saa kabla ya kuanza kazi. Kama unafanya kazi ya taaluma uliyosomea lakini maisha hayaendi, fikiria kubadili mwelekeo wa maisha ikiwemo taaluma kufikia malengo uliyojiwekea.
Enock Maregesi Quote #11
Be nice to the environment. Be nice to animals. Be nice to people. If you do that, you will leave a mark on the world.
Enock Maregesi Quote #12
Bibi Martha Maregesi aliishi maisha mazuri sana hapa duniani. Alibarikiwa na Mungu. Aliishi miaka 84 – siku 30660 badala ya siku 25550 tulizopangiwa na Mungu. Katika uhai wake wote, kwa wale wote aliowalea, hakuna mtoto wake hata mmoja aliyefariki kabla yake. Hakuna mjukuu wake hata mmoja aliyefariki kabla yake. Hakuna kitukuu chake hata kimoja kilichofariki kabla yake. Bibi yangu ametimiza mwaka mmoja kamili leo hii, tangu amefariki dunia Novemba 4 mwaka 2014 mjini Musoma. Tunamkumbuka leo akiwa amefariki kama tulivyomkumbuka jana akiwa hai. Nguvu ya sala zetu imfanye Mwenyezi Mungu aendelee kumsamehe dhambi zake zote, na amweke mahali anapostahili, Amina.
Enock Maregesi Quote #13
Binti yako mwenye umri wa miaka kumi na nne kwa mfano, anaomba umnunulie gari kama ulivyofanya kwa kaka yake mwenye umri wa miaka kumi na nane. Mara ya kwanza unamwambia utamnunulia atakapofikisha umri wa miaka kumi na nane kama ulivyofanya kwa kaka yake. Lakini baada ya wiki moja binti yako anakuomba tena kitu kilekile, yaani gari. Utajisikiaje? Utakereka, sivyo? Jinsi utakavyokereka binti yako kukuomba kitu ambacho tayari ameshakuomba, ndivyo Mungu anavyokereka sisi kumwomba vitu ambavyo tayari tumeshamwomba. Ukiomba kitu kwa mara ya kwanza Mungu amekusikia, tayari ameshaandaa malaika wa kukuletea jibu. Unachotakiwa kufanya, baada ya kuomba, shukuru mpaka jibu lako litakapofika. Mungu huthamini zaidi maombi ya kushukuru kuliko maombi ya kuomba. Binti yako anachotakiwa kufanya baada ya kukuomba gari ni kukushukuru mpaka gari yake itakapofika, si kukuomba mpaka gari yake itakapofika.
Enock Maregesi Quote #14
Debbie alikuwa akimwangalia Murphy kama paka anavyoangalia maziwa.
Enock Maregesi Quote #15
Dunia ni uwanja wa vita wa vita ya dhambi ya vita ya maisha! Kuishi maisha ya kufikirika ni kushinda vita ya maisha ya vita ya dhambi. Vita ya dhambi ya vita ya maisha si vita ya kufikirika! Bila Yesu katika maisha yetu hakuna atakayeishinda.
Enock Maregesi Quote #16
Falsafa ya Usawa kwa Watu na Vitu Vyote ya Yin-Yang ya Kichina ni falsafa inayotumiwa na Wachina, kujifunza sanaa ya mapigano na kutengeneza madawa ya asili, na magaidi wa madawa ya kulevya wa Amerika ya Kusini na Kaskazini kusaidia watu waliosahauliwa na serikali zao.
Enock Maregesi Quote #17
Familia yako haikusaidii chochote katika mipango ya takdiri yako. Hii inasikitisha sana. Unajitahidi kila siku kuwafurahisha watu unaowapenda na watu wako wa karibu. Kila ukijitahidi kupata kibali cha watu unaishia kudharaulika na kuonekana mjinga asiyekuwa na maana. Sikiliza mazungumzo ya ndani ya moyo wako. Wapendwa wako watakukubali kama mtu hodari asiyekata tamaa, na tena watakuheshimu kutokana na tabia zako hizo. Mabadiliko haya ya kifikra hayatatokea haraka kama unavyofikiria. Yatachukua muda. Hivyo, kuwa mvumilivu. Wakati huohuo, endelea kucheza ngoma uliyoianzisha mwenyewe, endelea na mipango yako kama akili yako inavyokutuma.
Enock Maregesi Quote #18
Fanya kazi kwa bidii na maarifa!
Enock Maregesi Quote #19
Fikiri kama anavyofikiri tajiri. Ukifikiri tofauti na anavyofikiri tajiri, utakufa maskini.
Enock Maregesi Quote #20
Fikiria kwanza maana ya kitu unachofikiria, halafu tenda. Fikiria kwanza maana ya kitu unachosema, halafu sema.
Enock Maregesi Quote #21
Fikiria kwanza maana ya unachosema. Halafu sema.
Enock Maregesi Quote #22
Ford Bronco ilikuwa sehemu ya upelelezi wa polisi wa Tume ya Dunia, na ilipigwa mnada baada ya upelelezi na kesi kumalizika. Kiasi kikubwa cha pesa iliyopatikana kilikwenda kwa WPD – Idara ya Polisi ya Tume ya Dunia – ili iendelee kuimarisha huduma ya kukomesha biashara haramu ya madawa ya kulevya duniani.
Enock Maregesi Quote #23
Gari ya Debbie huchukua sekunde 12 kutoka kilometa 0 mpaka kilometa 210 kwa saa. Huchukua sekunde 10 kutoka kilometa 210 kwa saa mpaka kilometa 0. Ina uwezo wa kusimama haraka kuliko inavyoweza kukimbia.
Enock Maregesi Quote #24
Geuza hasira yako kuwa hekima.
Enock Maregesi Quote #25
Hadithi ya maisha yangu ni yangu. Wewe ni nani kusema hadithi yangu si ya kweli?
Enock Maregesi Quote #26
Hakuna maana yoyote kupambana na Shetani katika dunia hii ambapo yeye ndiye mtawala. Pambana na Shetani katika dunia ya kiroho ambapo Shetani hana nguvu yoyote dhidi ya Yesu Kristo.
Enock Maregesi Quote #27
Hakuna mtu mwenye akili timamu anayetaka mabaya katika maisha yake. Mwanamume atake mwanamke mwenye matendo mema. Mwanamke atake mwanamume mwenye matendo mema. Misingi ya hasanati ni misingi ya utu. Tukiishi katika misingi ya utu, misingi ya matendo mema, tutaishi sawasawa na mapenzi ya Mungu. Kila mtu anapaswa kuishi na mke au mume aliye mwema.
Enock Maregesi Quote #28
Hakuna shaka yoyote (kwa mfano) kwamba mboga za majani na matunda vina vitamini nyingi mwilini na madini na vitu vyote vizuri katika mwili wa binadamu, na kwamba kadhalika vina kirutubisho cha ufumwele ambacho huzuia kufunga choo na matatizo mengine ya mfumo wa usagaji chakula. Kirutubisho hiki kikizidi mwilini utapata matatizo makubwa yatakayoweza hata kukusababishia kifo!
Enock Maregesi Quote #29
Halafa hailipi.
Enock Maregesi Quote #30
Hasanati ni matendo mema. Mema yanatoka kwa Mungu. Mabaya yanatoka kwa Shetani. Mke mwema anatoka kwa Mungu. Mke mbaya anatoka kwa Shetani. Mke mwema ana hekima na busara, ana maadili na tabia njema, ana utu na uchapakazi, ana wema na upendo, na ana aibu kwa wanaume.
0 comments:
Post a Comment